Furahia Shangwe la Sikukuu na TANAPA kwa safari ya kipekee ya siku 2 na usiku 1 katika Hifadhi ya Taifa Nyerere kutokea Dar es Salaam. Huu ni wakati wa kupata uzoefu wa kusisimua wa kupiga kambi (camping) katikati ya pori la asili kwa gharama nafuu sana kuliko kulala hotelini.
Usiku wako utapambwa na sauti za viumbe wa porini na anga lenye nyota nyingi, hali inayotoa muunganisho wa karibu na asili.
Siku ya kwanza, utafurahia safari na mandhari ya mtoni Rufiji na game drive ya alasiri, kisha kulala kwenye hema zako salama.
Siku ya pili utamalizia na utalii wa asubuhi kabla ya kurejea Dar es Salaam. Camping inakupa uhuru na kumbukumbu zisizofutika kwa bei rafiki kwa mfuko wako.
Siku ya 1 Asubuhi: Kundoka Dar es Salaam kuelekea Hifadhi ya Nyerere mapema, kufika mchana, na kuelekee kambini.
Siku ya 1 Mchana: Kufurahia safari na mandhari nzuri ya kusisimua ya mto Rufiji.
Siku ya 1 Usiku: Kupiga kambi porini, chakula cha jioni, na kufurahia sauti za asili usiku kucha.
Siku ya 2 Asubuhi: Kuamka mapema, kufanya utalii wa asubuhi (game drive), na kisha kuanza safari ya kurejea Dar es Salaam.
Siku ya 2 Mchana: Kuwasili Dar es Salaam jioni.