Sherehekea Boxing Day kwa safari ya kusisimua ya siku moja kutoka Arusha Mjini kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara, ikiwa ni sehemu ya Kampeni ya Shangwe la Sikukuu na TANAPA – Msimu wa Pili. Safari hii inakupa nafasi ya kutoroka pilika za mjini na kuingia moja kwa moja kwenye uzuri wa asili, ukifurahia mandhari ya bonde la ufa, Ziwa Manyara na wanyamapori maarufu. Kwa mpango mzuri, safari fupi na gharama nafuu kwa watalii wa ndani, hii ni chaguo bora kwa familia, makundi ya marafiki na mtu yeyote anayetamani kuifanya siku ya sikukuu iwe ya kipekee na ya kukumbukwa. Karibu Arusha – Karibu Shangwe la Sikukuu!
Date: 26 Dec 2025 - 26 Dec 2025
1:30 Asubuhi
Kuondoka Arusha kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara
3:30 Asubuhi
Kuwasili getini, taratibu za kuingia hifadhini na mapumziko mafupi
4:00 – 7:00 Mchana
Game Drive ya kwanza ndani ya hifadhi – fursa ya kuona Tembo, Twiga, Nyati, Viboko, Swala, Nyani na Simba, pamoja na mandhari ya kuvutia ya Ziwa Manyara
7:00 – 8:00 Mchana
Mapumziko ya chakula cha mchana (Picnic Lunch) ndani ya hifadhi
8:00 – 10:00 Jioni
Kuendelea na Game Drive na kupiga picha za kumbukumbu
10:00 Jioni
Kuondoka hifadhini na kuanza safari ya kurejea Arusha
12:30 – 1:00 Jioni
Kuwasili Arusha Mjini na hitimisho la safari