uk-flag EN

26 Dec. - Boxing Day Trip to Arusha National Park (kuanzia Moshi Mjini)

1 day
Pick-up Point: Fresh Coach Restaurant, Posta

About the Safari

Safari Siku ya Boxing Day, kutembelea Hifadhi ya Kitaifa ya Arusha, kwa utulivu bila msongamano, ukiwa na Familia, Ndugu, Jamaa, na Marafiki. Siku hiyo itajumuisha kuona wanyama kwa gari tukipita misitu na savana, wanyama kama Twiga, Nyati na Tumbili adimu wa Colobus weusi na weupe. Utafurahia mandhari ya kuvutia ya Mlima Meru na maziwa maridadi ya Momella, nyumbani kwa ndege wengi, ikiwemo korongo maridadi.

Date: 26 Dec 2025 - 26 Dec 2025

26 Dec. - Boxing Day Trip to Arusha National Park (kuanzia Moshi Mjini)

Package Inclusions

  • Usafiri wenye hadhi (4x4 Safari Cruiser au Coaster) pamoja na Dereva/Guide mwenye uzoefu
  • Malipo ya kuingia hifadhini (Park Entry Fees)
  • Game Drive ndani ya Hifadhi kwa muda wote wa siku
  • Chakula cha Mchana (Picnic Lunch) na Maji ya Kunywa
  • Tozo za Serikali na Kodi husika

Package Exclusions

  • Vitu binafsi (kama vile vinywaji vya ziada pombe na ununuzi wa zawadi)
  • Bima ya Afya au Usafiri
  • Zawadi/Ada za Hiari (tips) kwa Dereva na Waongoza Wageni
  • Huduma zisizo kwenye mpangilio wa safari

Itinerary

Saa 12:00 Asubuhi. Kukutana na dereva/guide mjini Moshi. Maelezo mafupi ya safari na kuanza safari kwa gari kuelekea hifadhini (saa 2 kwa gari).

Saa 2:00 – 2:15 Asubuhi. Kufika lango la kuingilia Arusha National Park. Taratibu za kuingia na maandalizi ya Game Drive.

Saa 2:15 – 7:00 Mchana. Game Drive ya Asubuhi. Kutazama mandhari ya hifadhi na Maziwa ya Ngurdoto Kreta. Makundi makubwa ya Twiga, Tembo, Nyati, Pundamilia, Swala na Wanyama wengine.

Saa 7:00 – 8:00 Mchana. Chakula cha mchana (picnic lunch) katika eneo maalumu la mapumziko. Mapumziko mafupi huku ukifurahia mandhari na wanyama waliopo karibu.

Saa 8:00 – 10:00 Jioni. Walking Safari. Utalii wa Kutembea kwa Miguu, kuendelea kuchunguza sehemu nyingine za hifadhi. Kutembelea Maporomoko ya Maji, kupiga picha na kufurahia upekee wa mazingira ya Hifadhi ya Taifa ya Arusha.

Saa 10:00 – 12:00 Jioni. Safari ya kurejea mjini Moshi na kumaliza safari

Available Vehicle(s)

7-seater
🚐 7-seater
Toyota Land Cruiser LC 7SX
TZS 175,000 per person
Remaining Seats: 7 / 7
Book
29-seater
🚌 29-seater
Toyota Coaster
TZS 65,000 per person
Remaining Seats: 29 / 29
Book
Link copied to clipboard