Safari ya kipekee ya Siku ya Boxing Day, kutembelea Hifadhi ya Kitaifa ya Arusha, kwa utulivu bila msongamano. Siku hiyo itajumuisha kuona wanyama kwa gari tukipita misitu na savana, wanyama kama Twiga, Nyati na Tumbili adimu wa Colobus weusi na weupe. Utafurahia mandhari ya kuvutia ya Mlima Meru na maziwa maridadi ya Momella, nyumbani kwa ndege wengi, ikiwemo korongo maridadi. Hifadhi hii pia inatoa fursa za kufanya safari za kutembea kwa miguu, hivyo kukupa mwonekano wa karibu zaidi wa asili.
Safari itaanzia na kumalizikia: Shoppers (TFA) - Arusha
Date: 26 Dec 2025 - 26 Dec 2025
Saa 1:00 Asubuhi. Kukutana na dereva/guide mjini Arusha. Maelezo mafupi ya safari na kuanza safari kwa gari kuelekea hifadhini (saa 1 kwa gari).
Saa 2:00 – 2:15 Asubuhi. Kufika lango la kuingilia Arusha national Park. Taratibu za kuingia na maandalizi ya Game Drive.
Saa 2:15 – 7:00 Mchana. Game Drive ya Asubuhi. Kutazama mandhari ya hifadhi na Maziwa ya Ngurdoto Kreta. Makundi makubwa ya Twiga, Tembo, Nyati, Pundamilia, Swala na Wanyama wengine.
Saa 7:00 – 8:00 Mchana. Chakula cha mchana (picnic lunch) katika eneo maalumu la mapumziko. Mapumziko mafupi huku ukifurahia mandhari na wanyama waliopo karibu.
Saa 8:00 – 10:00 Jioni. Game Drive ya Mchana. Kuendelea kuchunguza sehemu nyingine za hifadhi. Kuona ndege wakicheza katika maji ya ziwani. Kupiga picha na kufurahia upekee wa mazingira ya Hifadhi ya Taifa ya Arusha.
Saa 10:00 – 10:30 Jioni. Kuelekea nje ya hifadhi kupitia lango.
Saa 12:30 Jioni. Kurejea mjini Arusha na kumaliza safari