Safari hii ya siku moja kwenda Tarangire National Park ni chaguo bora kwa wasafiri wanaotaka kufurahia mandhari na wanyamapori wa kipekee ndani ya muda mfupi. Hifadhi hii inajulikana sana kwa makundi makubwa ya Tembo, Mibuyu Mikubwa yenye umri wa maelfu ya miaka, pamoja na Mto Tarangire unaovutia wanyama wengi hususan wakati wa kiangazi. Utapata nafasi ya kuona wanyamapori mbalimbali akiwemo Simba, Chui, Fisi, Swala, Nyati, Pundamilia na mamia ya ndege wa aina tofauti.
Safari itaanzia TFA Complex - Shoppers, Arusha
Date: 14 Oct 2025 - 14 Oct 2025
Saa 1:00 Asubuhi. Kukutana na dereva/guide mjini Arusha. Maelezo mafupi ya safari na kuanza safari kwa gari kuelekea Tarangire (saa 2–2.5 kwa gari).
Saa 3:30 – 4:00 Asubuhi. Kufika lango la kuingilia Tarangire. Taratibu za kuingia na maandalizi ya Game Drive.
Saa 4:00 – 7:00 Mchana. Game Drive ya Asubuhi. Kutazama mandhari ya miti ya Mibuyu na Mto Tarangire. Makundi makubwa ya Tembo, Nyati, Pundamilia, Swala na Wanyama wengine. Fursa ya kuona Simba, Chui au Fisi wakipumzika chini ya kivuli.
Saa 7:00 – 8:00 Mchana. Chakula cha mchana (picnic lunch) katika eneo maalumu la mapumziko. Mapumziko mafupi huku ukifurahia mandhari na wanyama waliopo karibu.
Saa 8:00 – 10:00 Jioni. Game Drive ya Mchana. Kuendelea kuchunguza sehemu nyingine za hifadhi. Kuona wanyamapori wakielekea kunywa maji mtoni. Kupiga picha na kufurahia upekee wa mazingira ya Tarangire.
Saa 10:00 – 10:30 Jioni. Kuelekea nje ya hifadhi kupitia lango.
Saa 12:30 Jioni. Kurejea mjini Arusha na kumaliza safari.