"Bata" la Drapperz Empire baada ya Arusha Auto Show 2026
Jiunge na Drapperz Empire wote katika safari hii ya kitalii ya siku moja kuelekea Makuyuni Wildlife Park, tukifurahia kwa pamoja kama ndugu, jamaa, marafiki na wana-familia ya Drapperz
Date: 13 Sep 2026 - 13 Sep 2026
Saa 1:00 Asubuhi – Kukutana eneo la kuondokea.
Saa 1:30 Asubuhi – Kuondoka kuelekea Makuyuni Wildlife Park.
Saa 2:30 Asubuhi – Kuwasili hifadhini, mapokezi na maelekezo ya usalama.
Saa 3:00 Asubuhi – Saa 5:30 Asubuhi – Safari ya kutazama wanyamapori (Game Drive), ikiwa ni pamoja na Choroa (Oryx), Twiga, Pundamilia, Swala mbalimbali, Nyumbu na aina nyingi za ndege wa porini.
Saa 5:30 Asubuhi – Saa 6:00 Mchana – Muda wa kupiga picha na kupumzika katika maeneo maalum yenye mandhari nzuri.
Saa 6:00 Mchana – Saa 8:00 Alasiri – Chakula cha mchana na Game Meat BBQ Experience (Nyamachoma Pori); fursa ya kipekee ya kuonja nyama mbalimbali za porini huku mkifurahia muziki, mazungumzo na washiriki wa Arusha Auto Show.
Saa 8:00 Alasiri – Saa 9:00 Alasiri – Burudani, picha za pamoja na muda wa mapumziko.
Saa 9:00 Alasiri – Kuanza safari ya kurejea Arusha.
Saa 10:00 Jioni – Kuwasili Arusha na kuhitimisha safari.