Hifadhi ya Makuyuni inajulikana kwa kutokuwa na msongamano na inatoa fursa nzuri ya kuona wanyama kwa uhakika.
Hifadhi ya Wanyamapori ya Makuyuni inatoa fursa ya pekee ya safari ya siku moja yenye utulivu, ikifanya kazi kama korido muhimu ya uhamaji wa Tembo na kuwa makazi ya wanyama wengine kama Twiga, Pundamilia, na Kudu. Furahia Game Drive ya asubuhi yenye kusisimua, na upande Kilima cha Kipara kwa mtazamo wa kuvutia, huku ukipata uzoefu wa karibu na asili bila msongamano.
Date: 26 Dec 2025 - 26 Dec 2025
1. 12:00 Asubuhi: Kuondoka Moshi (Pickup)
2. 12:00 - 03:00 Asubuhi: Safari Kuelekea Makuyuni Wildlife Park kupitia Arusha (Breakfast)
3. 03:30 Asubuhi: Kuingia Hifadhini na kuanza Game Drive ya Asubuhi
4. 07:00 Mchana: Chakula cha Mchana (Bush Picnic Lunch)
5. 08:00 – 9:30 Alasiri: Game Drive ya Mchana
6. 10:00 Jioni: Kuondoka Makuyuni Wildlife Park
7. 1:30 Jioni: Kufika Moshi (Drop-off)