Ziara ya siku moja kwenda Makuyuni Wildlife Park siku ya Sikukuu ya MWAKA MPYA 2026 ni fursa adimu na rahisi sana ya kuadhimisha siku hii maalum kwa kuzama kwenye asili ya pori la Afrika.
Ikiwa umbali wa takriban saa 3 tu kutoka Moshi, Makuyuni inafanya kazi kama korido muhimu ya wanyama kati ya Tarangire na Manyara, hivyo kuhakikisha wageni wanaona makundi ya Tembo, Twiga, Pundamilia, na Simba wakitembea katika mandhari ya Savannah.
Ukiwa katika hifadhi hii unaweza kufurahia Game Drive, kufanya Walking Safari kwa miguu, kupanda Kipara Hill kwa mtazamo wa kuvutia, na hata kutembelea kijiji cha Wamaasai jirani kwa uzoefu wa kitamaduni.
Kwa kuwa Mwaka Mpya ni siku ya mapumziko, inarahisisha kupanga safari hii vizuri, na utulivu wake, tofauti na msongamano wa mbuga nyingine, unaiweka Makuyuni kuwa chaguo bora la kutumia siku ya kwanza ya Mwaka 2026.
Date: 1 Jan 2026 - 1 Jan 2026
1. 12:00 Asubuhi: Kuondoka Moshi (Pickup)
2. 12:00 - 03:00 Asubuhi: Safari Kuelekea Makuyuni Wildlife Park kupitia Arusha (Breakfast)
3. 03:30 Asubuhi: Kuingia Hifadhini na kuanza Game Drive ya Asubuhi
4. 07:00 Mchana: Chakula cha Mchana (Bush Picnic Lunch)
5. 08:00 – 9:30 Alasiri: Game Drive ya Mchana
6. 10:00 Jioni: Kuondoka Makuyuni Wildlife Park
7. 1:30 Jioni: Kufika Moshi (Drop-off)