Anza mwaka Mpya wa 2026 ukiwa Hifadhi ya Taifa ya Tarangire. Safari hii ya siku moja itakupa fursa ya kujionea mandhari nzuri ya mto Tarangire, Mibuyu mikubwa, makundi makubwa ya Tembo, Ndege na Wanyama wengi unaposherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya na familia, ndugu, jamaa, na marafiki.
Safari Itaanzia & Kumalizikia: Shoppers (TFA) - Arusha
Date: 1 Jan 2026 - 1 Jan 2026
Saa 12:00 Asubuhi. Kukutana na dereva/guide mjini Arusha. Maelezo mafupi ya safari na kuanza safari kwa gari kuelekea Tarangire (saa 2–2.5 kwa gari).
Saa 2:30 – 3:00 Asubuhi. Kufika lango la kuingilia Tarangire. Taratibu za kuingia na maandalizi ya Game Drive.
Saa 3:00 – 7:00 Mchana. Game Drive ya Asubuhi. Kutazama mandhari ya miti ya Mibuyu na Mto Tarangire. Makundi makubwa ya Tembo, Nyati, Pundamilia, Swala na Wanyama wengine. Fursa ya kuona Simba, Chui au Fisi wakipumzika chini ya kivuli.
Saa 7:00 – 8:00 Mchana. Chakula cha mchana (picnic lunch) katika eneo maalumu la mapumziko. Mapumziko mafupi huku ukifurahia mandhari na wanyama waliopo karibu.
Saa 8:00 – 10:00 Jioni. Game Drive ya Mchana. Kuendelea kuchunguza sehemu nyingine za hifadhi. Kuona wanyamapori wakielekea kunywa maji mtoni. Kupiga picha na kufurahia upekee wa mazingira ya Tarangire.
Saa 10:00 – 10:30 Jioni. Kuelekea nje ya hifadhi kupitia lango.
Saa 12:30 Jioni. Kurejea mjini Arusha na kumaliza safari.