Sherehekea Mwaka Mpya 2026 kwa kutembelea Hifadhi ya Kitaifa ya Arusha ukiwa na Familia, Ndugu, Jamaa na Marafiki zako. Siku itajumuisha kuona wanyama kwa gari na kwa matembezi ya miguu (Walking Safari) tukipita misitu na savana, wanyama kama Twiga, Nyati na Tumbili adimu wa Colobus weusi na weupe. Utafurahia mandhari ya kuvutia ya Mlima Meru na maziwa maridadi ya Momella, nyumbani kwa ndege wengi. Safari yaa kutembea kwa miguu itakupa mwonekano wa karibu zaidi wa asili.
Date: 1 Jan 2026 - 1 Jan 2026
Saa 1:30 Asubuhi. Kukutana na dereva/guide mjini Arusha. Maelezo mafupi ya safari na kuanza safari kwa gari kuelekea hifadhini (nusu saa kwa gari).
Saa 2:00 – 2:15 Asubuhi. Kufika lango la kuingilia Arusha National Park. Taratibu za kuingia na maandalizi ya Game Drive.
Saa 2:15 – 7:00 Mchana. Game Drive ya Asubuhi. Kutazama mandhari ya hifadhi na Maziwa ya Ngurdoto Kreta. Makundi makubwa ya Twiga, Tembo, Nyati, Pundamilia, Swala na Wanyama wengine.
Saa 7:00 – 8:00 Mchana. Chakula cha mchana (picnic lunch) katika eneo maalumu la mapumziko. Mapumziko mafupi huku ukifurahia mandhari na wanyama waliopo karibu.
Saa 8:00 – 10:00 Jioni. Walking Safari. Utalii wa Kutembea kwa Miguu, kuendelea kuchunguza sehemu nyingine za hifadhi. Kutembelea Maporomoko ya Maji, kupiga picha na kufurahia upekee wa mazingira ya Hifadhi ya Taifa ya Arusha.
Saa 10:00 – 11:00 Jioni. Safari ya kurejea mjini Arusha na kumaliza safari