Jumamosi ya Kwanza ya Mwaka Mpya 2026 ni ishara ya mwanzo mpya, matumaini na bahati njema—na hakuna njia bora kwa mtalii kuianza siku hii kuliko safari ya siku moja kwenda Lake Manyara National Park. Kutembea ndani ya hifadhi siku hii ya kipekee huaminika kuwa alama ya bahati, baraka na safari njema kwa mwaka mzima, ukianza mwaka katikati ya asili, utulivu na uzuri usio na kifani.
Date: 3 Jan 2026 - 3 Jan 2026
1:30 Asubuhi
Kuondoka Arusha kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara
3:30 Asubuhi
Kuwasili getini, taratibu za kuingia hifadhini na mapumziko mafupi
4:00 – 7:00 Mchana
Game Drive ya kwanza ndani ya hifadhi – fursa ya kuona Tembo, Twiga, Nyati, Viboko, Swala, Nyani na Simba, pamoja na mandhari ya kuvutia ya Ziwa Manyara
7:00 – 8:00 Mchana
Mapumziko ya chakula cha mchana (Picnic Lunch) ndani ya hifadhi
8:00 – 10:00 Jioni
Kuendelea na Game Drive na kupiga picha za kumbukumbu
10:00 Jioni
Kuondoka hifadhini na kuanza safari ya kurejea Arusha
12:30 – 1:00 Jioni
Kuwasili Arusha Mjini na hitimisho la safari