Mgahawa wa Kulan Restaurant unawaalika wateja wake katika safari maalum ya siku moja kwenda Makuyuni Wildlife Park kama sehemu ya kufurahi pamoja, kujenga ukaribu na kutoa shukrani kwa uaminifu na uungwaji mkono wenu. Safari hii itajumuisha matembezi ya kutazama mandhari nzuri, wanyama pori na kutumia muda wa pamoja katika mazingira ya asili yanayotuliza. Kipengele cha kipekee cha safari hii ni Nyama Pori Choma, itakayoandaliwa kwa ustadi kama zawadi na shukrani kwa wageni wote watakaoshiriki. Ni nafasi ya kupumzika, kushirikiana, na kuunda kumbukumbu nzuri kati ya Kulan Restaurant na wateja wake wapendwa. Karibuni tufurahie siku hii maalum kwa pamoja tunapoanza mwaka 2026.!
Date: 4 Jan 2026 - 4 Jan 2026
12:30 Asubuhi: Kuondoka Arusha (Pickup)
12:45 Asubuhi: Breakfast safarini Kuelekea Makuyuni Wildlife Park
02:30 Asubuhi: Kuingia Hifadhini na kuanza Game Drive ya Asubuhi
05:00 Asubuhi: Kufanya Utalii wa Kutembea ndani ya Hifadhi
06:00 Mchana: Chakula cha Mchana (Bush Picnic Lunch)
08:00 Mchana: Game Drive ya Mchana
10:00 Jioni: Kuondoka Makuyuni Wildlife Park
11:30 Jioni: Kufika Arusha (Drop-off)