Safari hii ya siku moja kwa gari ndani ya Arusha National Park itakupa nafasi ya kutembelea vivutio vikuu vya hifadhi hii. Utafurahia "Game Drive" kupitia mandhari ya kipekee ya Ngurdoto Crater, Momella Lakes na misitu ya kijani inayopendeza. Kwa muda wa siku moja tu, unaweza kushuhudia wanyama mbalimbali wakiwemo Twiga, Nyati, Nyani, Pofu, Nyumbu na Ndege wa aina nyingi akiwemo Flamingo. Ni safari rahisi, yenye starehe na inayotoa picha kamili ya uzuri wa Hifadhi ya Taifa ya Arusha kwa muda mfupi.
Safari itaanzia TFA Complex - Shoppers, Arusha
Date: 14 Oct 2025 - 14 Oct 2025
• Saa 1:30 Asubuhi
Kukutana na dereva/guide mjini Arusha.
Maelezo mafupi ya safari na kuanza safari kwa gari kuelekea hifadhini.
• Saa 2:30 – 3:00 Asubuhi
Kufika Ngongongare Gate (Lango wa kuingilia).
Taratibu za kuingia hifadhini na maandalizi ya Game Drive.
• Saa 3:00 – 6:30 Mchana
Game Drive ya Asubuhi
Kutembelea Ngurdoto Crater yenye mandhari ya kupendeza.
Kuona wanyama kama Twiga, Nyati, Nyumbu, Pofu, Nyani na Sokwe Wekundu.
Kutembelea Momella Lakes, maarufu kwa makundi ya ndege, wakiwemo Flamingo.
• Saa 6:30 – 7:30 Mchana
Chakula cha mchana (picnic lunch) katika eneo maalumu ndani ya hifadhi.
Mapumziko mafupi huku ukifurahia mandhari ya Mlima Meru na mazingira ya hifadhi.
• Saa 7:30 – 9:30 Alasiri
Kuendelea na Game Drive ya Mchana, ukichunguza sehemu tofauti za hifadhi na kufurahia mandhari ya asili na wanyamapori.
• Saa 9:30 – 10:00 Jioni
Kuelekea kwenye lango la kutoka hifadhini.
• Saa 11:00 Jioni
Kurejea mjini Arusha, kukamilisha safari.