Sherehekea Boxing Day kwa safari ya kipekee ya siku moja kutoka Moshi Mjini kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara, kama sehemu ya Kampeni ya Shangwe la Sikukuu na TANAPA – Msimu wa Pili. Safari hii inakupa fursa ya kufurahia uzuri wa asili, kuona wanyamapori maarufu kama Tembo, Twiga, Viboko na Simba-Wanaopanda-Miti, pamoja na mandhari ya kuvutia ya Ziwa Manyara.
Date: 26 Dec 2025 - 26 Dec 2025
11:00 Alfajiri
Kuondoka Moshi kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara
03:30 Asubuhi
Kuwasili getini, taratibu za kuingia hifadhini na mapumziko mafupi
4:00 – 7:00 Mchana
Game Drive ndani ya hifadhi – kuona Tembo, Twiga, Nyati, Viboko, Swala, Nyani na Simba-Wanaopanda-Miti, pamoja na mandhari ya kuvutia ya Ziwa Manyara
7:00 – 8:00 Mchana
Chakula cha Mchana (Lunch break) ndani ya hifadhi
8:00 – 10:00 Jioni
Kuendelea na Game Drive na kupiga picha za kumbukumbu
10:00 Jioni
Kuondoka hifadhini na kuanza safari ya kurejea Moshi kupitia Arusha
2:00 – 3:00 Usiku
Kuwasili Moshi Mjini na hitimisho la safari