Malizia Wikiendi ya Mwisho ya Mwaka 2026 kwa safari ya kipekee ya siku moja kutoka Moshi Mjini kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara, kama sehemu ya Kampeni ya Shangwe la Sikukuu na TANAPA – Msimu wa Pili. Safari hii inakupa fursa ya kufurahia uzuri wa asili, kuona wanyamapori maarufu kama Tembo, Twiga, Viboko na Simba-Wanaopanda-Miti, pamoja na mandhari ya kuvutia ya Ziwa Manyara.
Date: 28 Dec 2025 - 28 Dec 2025
11:00 Alfajiri
Kuondoka Moshi kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara
03:30 Asubuhi
Kuwasili getini, taratibu za kuingia hifadhini na mapumziko mafupi
4:00 – 7:00 Mchana
Game Drive ndani ya hifadhi – kuona Tembo, Twiga, Nyati, Viboko, Swala, Nyani na Simba-Wanaopanda-Miti, pamoja na mandhari ya kuvutia ya Ziwa Manyara
7:00 – 8:00 Mchana
Chakula cha Mchana (Lunch break) ndani ya hifadhi
8:00 – 10:00 Jioni
Kuendelea na Game Drive na kupiga picha za kumbukumbu
10:00 Jioni
Kuondoka hifadhini na kuanza safari ya kurejea Moshi kupitia Arusha
2:00 – 3:00 Usiku
Kuwasili Moshi Mjini na hitimisho la safari