Funga mwaka 2025 kwa utulivu, shukrani na bashasha kupitia safari ya siku moja kutoka Arusha Mjini kwenda Lake Manyara National Park katika Jumapili ya Mwisho wa Mwaka. Ni wakati muafaka wa kutafakari safari ya mwaka mzima, kushukuru kwa yote yaliyopita na kuaga mwaka ukiwa katikati ya uzuri wa asili, mandhari ya kuvutia ya Bonde la Ufa na wanyamapori. Safari hii ya Jumapili ya mwisho ni zaidi ya mapumziko—ni njia ya kifahari na yenye maana ya kufunga mwaka, kuacha mizigo ya jana na kujiandaa kuukaribisha mwaka mpya kwa moyo mweupe, matumaini mapya na kumbukumbu zisizosahaulika. Funga 2025 kwa amani na heshima.
Date: 28 Dec 2025 - 28 Dec 2025
1:30 Asubuhi
Kuondoka Arusha kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara
3:30 Asubuhi
Kuwasili getini, taratibu za kuingia hifadhini na mapumziko mafupi
4:00 – 7:00 Mchana
Game Drive ya kwanza ndani ya hifadhi – fursa ya kuona Tembo, Twiga, Nyati, Viboko, Swala, Nyani na Simba, pamoja na mandhari ya kuvutia ya Ziwa Manyara
7:00 – 8:00 Mchana
Mapumziko ya chakula cha mchana (Picnic Lunch) ndani ya hifadhi
8:00 – 10:00 Jioni
Kuendelea na Game Drive na kupiga picha za kumbukumbu
10:00 Jioni
Kuondoka hifadhini na kuanza safari ya kurejea Arusha
12:30 – 1:00 Jioni
Kuwasili Arusha Mjini na hitimisho la safari