Jumatatu ya Pasaka 2026 ndani ya Arusha National Park.
Day Trip kutembelea Hifadhi ya Kitaifa ya Arusha. Siku itajumuisha kuona wanyama kwa gari na kwa matembezi ya miguu (Walking Safari) tukipita misitu na savana, wanyama kama Twiga, Nyati na Tumbili adimu wa Colobus weusi na weupe. Utafurahia mandhari ya kuvutia ya Mlima Meru na maziwa maridadi ya Momella, nyumbani kwa ndege wengi. Safari yaa kutembea kwa miguu itakupa mwonekano wa karibu zaidi wa asili.
Date: 6 Apr 2026 - 6 Apr 2026
Saa 1:30 Asubuhi. Kukutana na dereva/guide mjini Arusha.
Saa 2:00 – 2:15 Asubuhi. Kufika lango la kuingilia Arusha National Park. Taratibu za kuingia na maandalizi ya Game Drive.
Saa 3:00 – 5:00 Asubuhi. Walking Safari. Utalii wa Kutembea kwa Miguu.
Saa 5:00 – 7:00 Mchana. Game Drive ya Asubuhi. Kutazama mandhari ya hifadhi na Maziwa ya Ngurdoto Kreta.
Saa 7:00 – 8:00 Mchana. Chakula cha mchana (picnic lunch) katika eneo maalumu la mapumziko.
Saa 9:00 – 11:00 Jioni. Game Drive ya Pili na safari ya kurejea mjini Arusha