Shirika la Hifadhi za Taifa - TANAPA - kwa kupitia Kampeni yake ya Shangwe la Sikukuu na TANAPA, linatoa fursa ya safari ya Mwaka Mpya si kama matembezi tu bali na uzoefu wa kiroho na kisaikolojia unaokupa fursa ya kuacha yaliyopita, kujiwekea malengo mapya na kuukaribisha mwaka kwa furaha, shukrani na matumaini mapya. Anza mwaka kwa hatua ya bahati—ndani ya moyo wa asili ya Tanzania.
Date: 1 Jan 2026 - 1 Jan 2026
1:30 Asubuhi
Kuondoka Arusha kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara
3:30 Asubuhi
Kuwasili getini, taratibu za kuingia hifadhini na mapumziko mafupi
4:00 – 7:00 Mchana
Game Drive ya kwanza ndani ya hifadhi – fursa ya kuona Tembo, Twiga, Nyati, Viboko, Swala, Nyani na Simba, pamoja na mandhari ya kuvutia ya Ziwa Manyara
7:00 – 8:00 Mchana
Mapumziko ya chakula cha mchana (Picnic Lunch) ndani ya hifadhi
8:00 – 10:00 Jioni
Kuendelea na Game Drive na kupiga picha za kumbukumbu
10:00 Jioni
Kuondoka hifadhini na kuanza safari ya kurejea Arusha
12:30 – 1:00 Jioni
Kuwasili Arusha Mjini na hitimisho la safari