Safari hii ya siku moja inafaa sana kufanywa tarehe 9 Desemba, ikiwa ni Siku Kuu ya Uhuru wa Tanzania, kwani likizo hii hurahisisha kupanga safari nzima, na hali ya hewa katika kipindi hiki mara nyingi hutoa mtazamo mzuri zaidi wa Mlima Meru na Mlima Kilimanjaro ulioko mbali.
Safari ya siku moja kwenda Hifadhi ya Taifa ya Arusha ni chaguo bora kabisa lililojaa shughuli, ikiwa umbali wa dakika 45 tu kutoka Arusha mjini.
Hifadhi hii inajulikana kwa utofauti mkubwa upande wa hifadhi za Kaskazini, ikitoa mchanganyiko wa kipekee wa shughuli tofauti na hifadhi nyingine zozote za jirani. Wageni wataona wanyama, msitu pori mnene wa milimani—ambapo hukaa kima wakubwa weusi na weupe (Colobus monkey)—pamoja na fursa ya kusisimua ya kutembea kwa miguu (Walking Safari) kuongozwa na askari mwenye silaha, na hivyo kukaribia Twiga, Nyati, na Pundamilia.
Siku hiyo pia inajumuisha vituo vya kutazama mandhari kwenye ukingo wa Kreta ya Ngurdoto na fursa ya kufanya safari tulivu ya mtumbwi (Canoe Safari) kwenye Maziwa ya Momella, yanayojulikana kwa idadi kubwa ya Flamingo.
Safari Itaanzia: Shoppers - Arusha
Date: 9 Dec 2025 - 9 Dec 2025
Saa 1:00 Asubuhi. Kukutana na dereva/guide mjini Arusha. Maelezo mafupi ya safari na kuanza safari kwa gari kuelekea hifadhini (saa 1 kwa gari).
Saa 2:00 – 2:15 Asubuhi. Kufika lango la kuingilia Arusha national Park. Taratibu za kuingia na maandalizi ya Game Drive.
Saa 2:15 – 7:00 Mchana. Game Drive ya Asubuhi. Kutazama mandhari ya hifadhi na Maziwa ya Ngurdoto Kreta. Makundi makubwa ya Twiga, Tembo, Nyati, Pundamilia, Swala na Wanyama wengine.
Saa 7:00 – 8:00 Mchana. Chakula cha mchana (picnic lunch) katika eneo maalumu la mapumziko. Mapumziko mafupi huku ukifurahia mandhari na wanyama waliopo karibu.
Saa 8:00 – 10:00 Jioni. Game Drive ya Mchana. Kuendelea kuchunguza sehemu nyingine za hifadhi. Kuona ndege wakicheza katika maji ya ziwani. Kupiga picha na kufurahia upekee wa mazingira ya Hifadhi ya Taifa ya Arusha.
Saa 10:00 – 10:30 Jioni. Kuelekea nje ya hifadhi kupitia lango.
Saa 12:30 Jioni. Kurejea mjini Arusha na kumaliza safari.