Anza Jumamosi ya Kwanza ya Mwaka 2026 kwa bashasha na baraka za kipekee kupitia safari ya siku moja kutoka Moshi Mjini kwenda Lake Manyara National Park. Inaaminika mwanzo mzuri huufanya mwaka mzima uwe na bahati njema—na hakuna mwanzo bora kuliko kuukaribisha mwaka mpya katikati ya uzuri wa asili, hewa safi na wanyamapori wa kuvutia. Safari hii ya Jumamosi ya kwanza si tu mapumziko, bali ni ishara ya baraka, matumaini na mafanikio kwa mwaka mzima—wakati wa kuacha yaliopita na kuukaribisha mwaka mpya kwa furaha, shukrani na kumbukumbu zisizosahaulika. Anza 2026 kwa hatua sahihi—ndani ya moyo wa asili ya Tanzania!
Date: 3 Jan 2026 - 3 Jan 2026
11:00 Alfajiri
Kuondoka Moshi kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara
03:30 Asubuhi
Kuwasili getini, taratibu za kuingia hifadhini na mapumziko mafupi
4:00 – 7:00 Mchana
Game Drive ndani ya hifadhi – kuona Tembo, Twiga, Nyati, Viboko, Swala, Nyani na Simba-Wanaopanda-Miti, pamoja na mandhari ya kuvutia ya Ziwa Manyara
7:00 – 8:00 Mchana
Chakula cha Mchana (Lunch break) ndani ya hifadhi
8:00 – 10:00 Jioni
Kuendelea na Game Drive na kupiga picha za kumbukumbu
10:00 Jioni
Kuondoka hifadhini na kuanza safari ya kurejea Moshi kupitia Arusha
2:00 – 3:00 Usiku
Kuwasili Moshi Mjini na hitimisho la safari